Thursday, 11 October 2018
RIDHIKENI
Salamu kwa kina dada, nimekuja kuwaponza
Nawaombeni wenu muda, hoja nipate kuzihonza
Lamu mpaka chuda, niwajuze kinacho nikinza
Itakuwaje mliwe na babu buda, ilihali rika zenu mwatulunza
Wakutosha ninao ushuhuda, wengi kuuliwa na sponsor
Kisa kulipia misaada, ya wao nyie kuwatunza
Obado Sharon wakavimbada, na kitoto mwisho kukifyonza
Nikiwapa Hii taarifa labda, mtapata kujifunza
Ridhikeni na hali zenu, sikimbilie paka mzee
Upatacho ngali finyu, mauti sijilimbikize
Ni hatari si fununu, kutoroka we jikaze
Madondo chapo ndio menu, 5 star sivizevize
Jowi na Monica, Habari hizi zishawafikia
Maskini na visu akadungika, bila hata kuhurumia
Kisa kudata daka, na yeyote anayemvizia
Jambo hili latia shaka, yaarabi najililia
Nasibu natapatapa, simanzi menikazia
Wino meshuka paa, sakafuni memalizia
Wachaneni na kina papa, mwisho wao kujutia
Kikomo nakieka hapa, siwafanye zidi kulia
Amazing work,,,,love it brother reality situation
ReplyDeleteNice one
ReplyDeleteShairi lililotungwa likatungika.Natumai itakuwa funzo kwa dada zetu walio mbali na mwangaza ili wafikie malengo yao.Shukrani Malenga Nasibu kwa kazi safi na Mungu akuzidishie heri njema na haraka.Asante sana
ReplyDeleteKuwachamba umewachamba tusubiri matokea tukitumai litakuwa funzo @halua ya mapenzi
DeleteInafunza kweli
DeleteGood job,amaizing article
DeleteGood job,amaizing article
Deletekongole, kazi nzuri
ReplyDeleteGreat piece brother.... So educative
ReplyDeleteGreat piece brother.... So educative
ReplyDelete